LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 9, 2019

DKT. BASHIRU AZUNGUMZA NA MABALOZI WA MASHINA MKOANI MOSHI


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amesema Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na mwenzake wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), wamekuwa wakifanyakazi ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.

Mbali na Mbatia, pia aliwataja wabunge Zitto Kabwe wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo) na Mchungaji Peter Msigwa  wa Iringa Mjini (Chadema).

Hayo aliliyasema mjini Moshi, alipokuwa akizungumza na mabalozi wa mashina ambapo alisema  wabunge hao wamekuwa wakifanyakazi ya chama tawala CCM kwa sababu hawana serikali wala Ikulu na kwasasa wanafanyakazi kwa maelekezo ya CCM.

Pamoja na hali hiyo, alitoa onyo kwa Zitto  ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na kusema si wa viwango vyake huku akimtaka kumtomzoea.

“Mbatia ni mtu mwelewa sana sisi kama chama tutakaa nae tumpe malekezo na kwamba hatuna wasiwasi nae kabisa. Msingwa pia na Zitto hawana shida wale ni watu wetu wanaisaidia CCM kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama .

“Mbowe  tutampa maelekezo,tunajua na jana nilikuwa jimboni kwake Hai , nilipokelewa vizuri na watu wake wameniahidi wako tayari,” alisema Dk. Bashiru.

Aliwataka wananchi waendelee kuchapa kazi ili kujenga uchumi wa nchi na katu waepuke kuishi maisha ya anasa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages