LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 4, 2019

MAANDAMANO YA WANANCHI YALAZIMISHA SERIKALI YA ALGERIA KUUNDA TUME YA MAZUNGUMZO YA KITAIFA

Baada ya kushadidi maandamano makubwa ya wananchi, rais wa muda wa Algeria amesema kuwa, kumeshaandaliwa mazingira ya kuanza mazungumzo ya kitaifa nchini humo.
Gazeti la al Shuruq limemnukuu Abdul Qadir bin Saleh akisema kuwa, ameunda tume maalumu ya watu huru kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kufanyika mazungumzo ya kitaifa na kuitishwa uchaguzi wa rais haraka iwezekanavyo.
Rais huyo wa muda wa Algeria ameongeza kuwa, hakuna hata mjumbe mmoja wa kamati anayetoka katika chama fulani cha kisiasa au anayependelea mrengo fulani na kazi yake ni kufanya uchunguzi wa kina na kuandaa mazingira ya kufanyika uchaguzi salama, huru na wa haki. 
Rais wa zamani wa Algeria aliyeng'olewa madarakani kwa maandamano ya wananchi

Maandamano makubwa ya wananchi wa Algeria yalimlazimisha rais wa zamani wa nchi hiyo, Abdelaziz Bouteflika ang'oke madarakani mapema mwezi Aprili mwaka huu na nafasi yake kuchukuliwa na Abdul Qadir bin Saleh anayeongoza serikali ya mpito.
Hata hivyo maandamano ya wananchi yanaendelea hadi hivi sasa kutaka wafuasi wote wa Bouteflika watolewe serikalini.
Hii ni katika hali ambayo, Luteni Jenerali Ahmed Gaid Salah, mkuu wa jeshi la Algeria amepinga utatuzi wowote wa mgogoro wa nchi hiyo usioheshimu sheria na kusema kuwa, jeshi linahimiza kuchukuliwa hatua za haraka za kuitishwa uchaguzi mkuu ulio salama na wa haki kwa mujibu wa sheria na katiba ya Algeria.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages