LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 5, 2019

IDADI YA VIFO VYA WAHAMIAJI YAFIKIA 53



Idadi ya vifo vilivyotokana na shambulizi katika kizuizi cha wahamiaji karibu na mji mkuu wa Libya Tripoli, imeongezeka na kufikia 53 huku watu wengine 130 wakijeruhiwa.

Shirika la afya duniani WHO, limesema vifo hivyo vya shambulio la Jumanne usiku kwa ujumla, vimefikia 1000 na majeruhi 5000 tangu kamanda Khalifa Haftar alipoanzisha mashambulizi katika mji mkuu wa Tripoli mwezi Aprili.

Msemaji wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, Joel Millman amesema watoto sita na angalau wahamiaji wawili waliokuwa waondoke wiki hii, chini ya mpango wa hiari wa kurejeshwa ni miongoni mwa waliouawa.

Mataifa tofauti 17 mengi ya Afrika, yalikuwa ni miongoni mwa wahamiaji 600 waliowakilishwa katika kizuizi cha Tajoura, amewaeleza waandishi wa habari mjini Geneva.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages