Na Frank Shija – MAELEZO, Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amempongeza Rais Uhuru Kenyatta
kwa kuwa Rais wa kwanza wa nje kutembelea Wilaya ya Chato.
Amesema kuwa
ukiachilia mbali ujirani uliopo baina ya Tanzania na Kenya, pia kuna undugu kwa
kuwa tunazungumza lugha moja, tunamuingiliano wa kijamii ikiwemo kuoana na kuwa
na utamaduni unaofanana.
“Kufika kwako umeudhihirishia
umma wa dunia kuwa sisi ni majirani, na marafiki wa kweli siku zote tutatembea
pamoja kamwe tusikubali kulaghaiwa na watu,” amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli amesema
kuwa kutokana na ushirikiano huo wafanyabiasha wa Kenya na Tanzania wamekuwa
wakishirikiana katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kijamii ikiwemo
kuwekeza katika nchi zetu.
Kwa mujibu wa takwimu
za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Kenya imewekeza miradi 504 yenye thamani
ya dola 1.7 biloni ikiwa na idadi ya watu 50,956 huku wawekezaji wa Tanzania
nchini Kenya wakiwa wakekezaji 24.
Aidha katika Sekta ya
Utalii, Tanzania ni nchi ya pili kwa watu wake kutembela nchini Kenya
ikitanguliwa na nchi ya Marekani ambapo kwa mujibu ya takwimu za Bodi ya utalii
ya Kenya ya Mwaka 2018 Watanzania 222,216 walitembelea Kenya ambayo ni zaidi ya
10% ya watu wote waliotembelea Kenya.
Katika hatua nyingine
Rais Magufuli ameitaja miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kwa ushirikiano
wan chi hizi mbili ikiwemo barabara ya Holili- Arusha hadi Namanga pamoja na
maandalizi ya ujenzi wa Barabara kutoka Mombasa hadi Bagamoyo.
Rais Magufuli amesema
kuwa Tanzania ipo katika hatua mbalimbali za kujenga meli tano ambapo
itaanzisha safari za kutoka Bukoba – Mwanza – Kisumu na Jinja.
Vile vile Rais Dkt. Magufuli
ametoa wito kwa wawekezaji kutoka Kenya kuja kuwekeza nchini hapa kwa kuwa
milango ipo wazi kwa mwekezaji yeyote na Watanzania waendelee kuwekeza Kenya
ili kuendeleza ushirikiano uliopo kwa mustakabari wa maendeleo ya nchi zote
mbili.
Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru
Kenyata amesema anayofuraha kuwa Rais wa kwanza wa nje kukanyaga ardhi ya
Chato.
Ameongeza kwamba uwepo
wake Chato Mkoani Geita ni udhibitisho kuwa nchi hizi ni ndugu na wapo kwa
ajili ya kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Kenya.
“Hakuna mtu anayeweza
kututenganisha kamwe, sisi kama watu wa Afrika Mashariki yatupasa kuhakikisha
tunaondoa vikwazo vyote vitakavyozuia kutembeleana, kufanyabiashara pamoja na
pengine hata kuoana.” Alisema Kenyatta.
Katika hatua nyingine Rais
Kenyatta ameipongeza Serikali kwa kujenga uwanja wa ndege wa Chato kwa kuwa ni
utaimarisha na kukuza ukuaji wa biashara na shughuli nyingine za kimaendelea
katika ukanda huo jambo ambalo halipaswi kubezwa.
Amesema anashangazwa
na baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakipuuza jitihada hizo za kujenga uwanja
huo kwani ni muhimu na yeye kama Rais wa Kenya angependa kuona Afrika ya
Mashariki inakuwa kitu kimoja.
Amechukizwa na kauli
za baadhi ya wanasiasa na kusema haiwezekani kumzuia Mtanzania kufanya biashara
au kuoa nchini Kenya vivyo hivyo kwa Wakenya nchini Tanzania.
Rais Kenyatta yupo
hapa nchini ikiwa ni ziara yake binafsi kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 05
Julai hadi siku ya kesho Jumamosi ya tarehe 06 Julai 2019.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇