LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 7, 2019

ALAANI VIKALI SHAMBULIO LA WAHAMIAJI LIBYA

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amelaani shambulizi la angani la mapema wiki hii lililosababisha vifo vya zaidi ya watu 50 katika kambi ya kuzuia wahamiaji nchini Libya.

Baada ya ibada ya Jumapili, Papa amesema kuwa jamii ya kimataifa haiwezi kuvumilia matukio mabaya kama hayo na kwamba anawaombea waathiriwa.

 Akiwahutubia waumini katika uwanja wa Mtakatifu Peter, Papa alitoa wito wa juhudi za pamoja katika hatua ya kibinadamu za kuwaondoa wahamiaji walio na mahitaji zaidi kutoka Libya.

 Aliwahimiza waumini kushirikiana naye katika muda wa ukimya kuwakumbuka waathiriwa wa mauaji ya kiholela ya hivi karibu nchini Afghanistan, Mali, Burkinafaso na Niger.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages