Na Amiri kilagalila
Jamii imeaswa kuacha unyanyasaji na ukatili kwa wakina mama na wasichana ili kuepusha vifo vitokanavyo na uzazi wakati wa kujifungua.
Wito huo umetolewa na mratibu wa muungano wa utepe mweupe Tanzania bi ROSE MLAY alipokuwa akiongea na mtandao huu leo June 13, 2019 baada ya semina waliyoitoa kwa watoa huduma ya jamii kutoka vituo mbalimbali vya kutolea huduma katika halmashauri ya wilaya Bukoba.
Amesema kuwa wanawake wamekuwa wakinyanyaswa pale walipokuwa wakienda kujifungua suala linalopelekea wengine kuchapwa na kufokewa na watoa huduma hali inayowafanya wakina mama hao kujisikia wapweke kwa manyanyaso hayo.
Amesema watoa huduma ya jamii wanaowajibu wa kuielimisha jamii kuhusu ukatili na wao kujiepusha na vitendo hivyo ili kuwapa uhuru wanawake kujifungua kwa amani na kuwatunzia usiri kwa kuwatengenezea faragha wakati wa kujifungua.
Aidha Mlay ameongeza kuwa watoto kuanzia miaka 14-17 wanaopata ujauzito katika umri huo hupoteza maisha mara 5 zaidi ya wanawake wenye umri zaidi ya huo ambapo vifo hivyo husababishwa na unyanyasaji kwa kuanzia Yule anaye mpa mimba hadi kwa mtoa huduma wakati wa kujifungua.
“Watoto hawa wamekuwa wakipoteza maisha wakiwa wajawazito na wengine wakati wa kujifungua kutokana na kufanyiwa unyanyasaji, tunaiomba jamii kukemea sana vitendo hivi ili kujenga jamii inayojielewa na kupinga ukatili kwa akina mama na wasichana.” Amesema Mlay.
Mlay amewasihi wakina baba kutowatelekeza wake zao wakati wa ujauzito kwa kwenda nao kriniki na hata siku ya kujifungua basi wawe nao katika chumba cha kujifungulia,ambapo amesema kuwa wakitengeneza ukaribu huo utwasaidia wakina mama kupuka vitendo vya ukatili.
Baadhi ya watoa huduma ya jamii waliohudhuria semina hii wamesema wanashukuru kwa kupata fursa ya kuongezewa uelewa kwa baadhi ya mambo ambayo walikuwa hawayajui na kuahidi kueneza elimu ya kuzuia ukatili ili kujenga jamii yenye ustawi bora.
Wameongeza kuwa wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali katika maeneo yao kubwa ikiwa ni mfumo dume uliopo kwenye jamii ambao huwapelekea kutelekezewa wakina mama wajawazito katika vituo vya kutolea huduma na waume zao.
Muungano wa utepe mweupe Tanzania umekuwa ukielimisha jamii juu ya vitendo vya ukatili kw awanawake na wasichana ambapo kwa moa Kagera wanaendelea kutoa elimu hiyo katika wilaya za Bukoba na Muleba.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇