LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 13, 2019

WAHIMIZWA WATOTO KUPATA CHANJO



Na Bilgither nyoni,Amiri kilagalila Njombe
                                         
Inaelezwa kuwa Ili  mtoto akue akiwa na afya bora anatakiwa apate chanjo zote muhimu za utotoni ambazo ndio msingi  mkuu wa kuzuia vifo vingi vya watoto,ukuaji mzuri na kuzuia kudumaa.

Kumekuwa na imani potofu kuhusu chanjo za watoto ambapo kuna baadhi ya wazazi wanashindwa kuwapeleka watoto wao kupata chanjo hata kama zinapatikana karibu yao ingawa chanjo hizo zinatolewa bila malipo, hivyo ni jukumu la mzazi kuhakikisha mtoto wake anapata chanjo zote kwa kukagua kadi yake ya kliniki.

Kwa kuzingatia hilo kituo hiki kimezungumza na Mratibu wa huduma za chanjo katika halmashauri ya mji wa Makambako Happiness martin, ambapo amesema chanjo ni jambo la lazima kwa kuwa linamlinda mtoto na hatari za kupata magonjwa ,Ulemavu wa kudumu au kupoteza maisha.

"faida mojawapo ni kuzuia magonjwa yanayozuiwa kwa chanjo,mfano pepo punda,surua,kifua kikuu,kifaduro,kupooza,kuharisha na hata saratani ya mlango wa kizazi,tuhudhurie katika vituo vya kutoa huduma ya chanjo kwa watoto kwa sababu kuna umuhimu mkubwa kwa watoto kuwakinga na magonjwa hayo"amesema Hapines martin

Kwa upande wake Mratibu msaidizi wa huduma za Chanjo katika halmashauri ya mji wa makambako Samwel vianga amesema  katika kuhakikisha huduma za chanjo zinawafikia watoto wote kuna vituo vimeanzishwa vijijini ili watoto wanaoishi mbali na mijini waweze kupatiwa chanjo hizo hivyo wazazi au walezi wanatakiwa kuwapeleka watoto kwenye vituo hivyo.

"kwa kweli sisi tuna vituo 9 vya mkoba ambavyo kwa wakazi walio mbali na mji wanashindwa kufika katika vituo huku mijini basi tunawafuata mpaka huko waliko ili tumfikie kila mtoto aweze kupata chanjo na kwa sababu huduma hii ni bure, na tunafanya hivyo  kwasababu swala hili sio la mji bali ni swala la kimkoa,kitaifa hata kidunia"amesema Samwel Vianga 

baadhi ya wakazi wa mji wa makambako licha ya kukiri umuhimu wa watoto kupata chanjo lakini wamesema elimu zaidi inahitajika kwa wazazi au walezi juu ya faida za watoto kupatiwa chanjo zote.

Hata hivyo shirika la afya duniani WHO Linakadilia kuwa watoto  milioni 19 duniani kote hawapati chanjo inayostahili ambapo zaidi ya watoto milioni 1 walio na umri chini ya miaka 5 hufariki kila mwaka kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuiwa kupitia chanjo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages