LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 13, 2019

TUHUMA ZA KUTUMWA SILAHA KATIKA NCHI ILIYOZINGIRWA

Mjumbe wa Baraza la Kisiasa la Harakati ya Answarullah nchini Yemen amesema kuwa, tuhuma za kutumwa silaha za kigeni ndani ya nchi hiyo ambayo imekuwa chini ya mzingiro wa kidhalimu na kuifanya ishindwe kudhamini mahitaji ya chakula na madawa, ni suala lisilofikirika na ni uongo wa wazi.
Ali Alqahoom ameyasema hayo katika mahojiano na Shirika la Habari la IRNA na kuongeza kwamba, kwa kuzingatia kuwa Yemen imekuwa chini ya uvamizi na mzingiro wa kila upande wa kidhalimu wa Saudia na Imarati katika pande tatu za nchi kavu, baharin na anga hivyo imekuwa  dharura kwa serikali ya wokovu wa kitaifa kustawisha na kutengeneza silaha za kistratijia, kwa madhumuni ya kuleta mlingano katika ulingo wa vita. Akizungumzia udharura wa kusambaratishwa uasi, kiburi na majivuno ya Imarati na Saudia amesema kuwa, akili na maandalizi ya Wayemen yamewaweza kutengeneza silaha zinazohitajika na kuwatwisha maadui mlingano katika vita.
Ali Alqhoom, Mjumbe wa Baraza la Kisiasa la Harakati ya Answarullah nchini Yemen
Kwa mujibu wa Ali Alqahoom kile ambacho maadui wanadai kwamba jeshi la Yemen limekipata kutoka nje ya nchi hiyo, ni njama za adui zilizoshindwa za kujaribu kufunika mafanikio na uwezo wa jeshi la Yemen mbele ya wavamizi. Wakati huo huo Mohamed Albakhitimjumbe wa Baraza la Kisiasa wa Harakati ya Answarullah amesema kuwa, vita alivyovianzisha Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia dhidi ya Yemen, havitakuwa na maslahi kwake. Albakhiti amebainisha kwamba kiwango cha uelewa cha raia wa Yemen, ni kati ya nukta za uwezo na dalili za ushindi wa serikali ya wokovu wa kitaifa nchini humo na kusisitiza kuwa siasa zilizopinda za 'udhaifu' mkabala wa siasa 'zenye nguvu' haziwezi kutekelezwa nchini Yemen. Jana Jumatano, kikosi cha mizinga cha jeshi la Yemen kwa kushirikiana na kamati za wananchi, kiliushambulia uwanja wa ndege wa Abha, kusini mwa Saudia kwa kombora la cruise na kupelekea kusimama shughuli zote za uwanja huo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages