LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 26, 2019

WAISHTAKI SAUDIA

Madada wa Afrika Kusini waishtaki Saudia UN kwa kuwazuilia na kuwatesa


Madada wawili wa Afrika Kusini ambao wamewahi kufungwa jela bila kufunguliwa mashitaka nchini Saudi Arabia wamewasilisha malalamiko yao kwa Umoja wa Mataifa.
Yumna Desai ambaye alikuwa mwalimu wa lugha ya Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Ha’il kaskazini mwa Saudia amesema utawala wa Riyadh ulimfunga katika gereza la Dhaban mjini Jeddah tokea mwaka 2015 hadi mwaka jana 2018. Binti huyo wa Afrika Kusini amesema mwaka mmoja na nusu baada ya kifungo hicho, utawala wa Aal-Saud ulimwambia kuwa amefungwa kutokana na hatia ambayo hakufafanuliwa, lakini iliyoelezwa kuwa ni jinai mitandaoni.
Dada yake kwa jina Huda Mohammad ambaye alikuwa ameolewa na raia wa Saudia na kuzaa naye binti mmoja, alifungwa jela mwaka mzima pasina kuambiwa shitaka lililokuwa likimkabili.
Mabinti hao wa Afrika Kusini wamesema ndugu zao wawili wa kiume pia walikamatwa na watawala wa Riyadh na kuzuiliwa kwa muda, lakini baadaye waliachiwa huru. Wanne hao walikuwa wakiishi na kufanya kazi nchini Saudia lakini hivi sasa wamesharejea nyumbani Afrika Kusini. 
Saudi imekuwa ikiwatesa wanawake wa ndani na nje ya nchi
Yumna Desai alitoa maelezo hayo pambizoni mwa kikao cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva jana Jumanne huku akibubujikwa na machozi.
Katika simulizi yake ya kusikitisha, binti huyo wa Afrika Kusini amebainisha kuwa, "Watu wanazuiliwa (nchini Saudia) kwa vipindi virefu huku wakiteswa na kudhalilishwa. Binafsi nilishuhudia watoto wakizuiliwa pamoja na wazazi wao. Niliona wanawake wanne wakijifungua ndani ya gereza."

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages