LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 26, 2019

MAGAIDI WA MAREKANI WAUAWA

Magaidi wa Marekani wauawa baada ya Pompeo kufanya safari ya kificho Afghanistan

Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi NATO umetangaza habari ya kuuawa askari magaidi wawili wa Marekani nchini Afghanistan leo Jumatano.
Kamandi ya uongozi wa majeshi ya Marekani na shirika la kijeshi la NATO imetoa taarifa ya kuthibitisha kuuawa askari wawili wa Marekani nchini Afghanistan lakini haikutoa ufafanuzi kuhusu kuuawa kwao.
Kwa mujibu wa NATO, wanajeshi tisa wa Marekani wameuawa tangu mwanzoni mwaka huu 2019 hadi sasa.
Mauaji hayo yamefanyika chini ya masaa 24, baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo kufanya safari ya kinyemela na kificho kikuu nchini humo. Amesema anatumai kuwa Marekani na kundi la Taliban zitafikia makubaliano ya amani kabla ya Septemba Mosi.
Aprili mwaka huu, msemaji wa kundi la Taliban, Dhabihullah Mujahid alisema kundi hilo limewaangamiza askari watano wa Marekani na wengine saba wamejeruhiwa nchini Afghanistan.
Askari vamizi wa Marekani nchini Afghanistan
Tangu Marekani ilipopeleka majeshi yake nchini Afghanistan mwaka 2001 hadi sasa, zaidi ya askari wake 2,400 wameuliwa na wengine wasiopungua 20,200 wamejeruhiwa.
Hii ni katika hali ambayo, wananchi wa Afghanistan wanapinga majeshi ya kigeni yakiongozwa na Marekani kuweko nchini mwao, na mara kadhaa wameitaka Washington ihitimishe uwepo wake kijeshi katika ardhi ya nchi hiyo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages