LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 26, 2019

BUNGE LAPITISHA BAJETI KUU YA SERIKALI YA SH. TRILIONI 33.1 KWA KISHINDO.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip  Mpango, akifanya majumuisho ya mjadala wa Bajeti Kuu ya mwaka 2019/20 kabla ya kupitishwa na Bunge, Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, akijibu hoja za Wabunge wakati wa majumuisho ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20 kabla ya kupitishwa kwa kishindo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashugwa akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizotolewa na Bunge wakati wa majumuisho ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20 kabla ya kupitishwa Bungeni Jijini Dodoma.
Dkt. Mpango na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji wakisikiliza kwa makini maelezo ya Mawaziri wakati wakijibu hoja mbalimbali za Wabunge kuhusu Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20, kabla ya kupitishwa Bungeni Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kushoto), akifurahia jambo wakati Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mpango (hayupo pichani), alipokua akifanya majumuisho ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2019/20.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwapongeza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mpango na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji, baada ya kufanya majumuisho ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20, kabla ya kupitishwa Bungeni Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (wa pili kushoto), akiwa na Wakuu wa Idara na Taasisi za Wizara hiyo wakifuatilia majumuisho ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20, kabla ya kupitishwa Bungeni Jijini Dodoma.
Baadhi ya Mawaziri na  Wabunge wakifurahia baada ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20 kuidhinishwa na Bunge Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wakiwapongeza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mpango  na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji, baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Sh. trilioni 33.1, katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
Dkt. Mpango (katikati), Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Ashatu Kijaji (wa tatu kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Doto James (wa pili kulia) na viongozi wengine, wakuu wa idara na Taasisi, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupitishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20, jijini Dodoma.(PICHA NA PETE HAULE NA JOSEPHINE MAJURA, WFM, DODOMA).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages