LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 19, 2019

WAIOMBA SERIKALI KUWATATULIA MGOGORO WA MIPAKA

Na. Enock Magali,Dodoma

Wananchi wa kata ya KeiKei wilayani Kondoa Mkoani Dodoma,wameiomba Serikali kuwatatulia kwa haraka mgogoro wa mipaka uliopo kati yao na pori la akiba la Mkungunero kwani mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu na wamekuwa wakishindwa kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo.
Wananchi hao wametoa malalamiko hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa, Dkt. Binilith Mahenge wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo,kuwasikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za wananchi.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara wananchi hao wamesema kuwa mgogoro huo umekuwa ni wa siku nyingi na wamekuwa wakiahidiwa kuletewa majibu ya utatuzi lakini muda unazidi kuyoyoma huku shughuli zao zikisimama.

"Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa,umekuja kutusikiliza,kero yetu kubwa sisi wana Keikei ni kuhusu huu mgogoro uliopo kati yetu na hifadhi,hadi sasa tuko njia panda hatulimi wala hatufugi,tunaomba utupatie ufumbuzi wa hili ili tuendelee na shughuli za kujiingizia kipato"Alisema mmoja wa wananchi.

Vilevile wananchi hao walidai kunyanyaswa kwa kupigwa na Askari wa pori hilo,pia kuchukuliwa mifugo yao pindi inapoonekana ikichunga ndani ya Pori jambo ambalo walidai kuwa ni uonevu mkubwa.

Akijibu kero hizo Mkuu wa Mkoa Dkt.Mahenge amewataka wananchi hao kuendelea kuwa na subra kwani Serikali inafanyia kazi mgogoro huo na hivi karibuni itakuja na utatuzi wa kudumu.

"Nafurahi mmenieleza na mimi mwenyewe nimesikia na kujionea changamoto hii kubwa mliyonayo wana Keikei,niwasihi tu,endeleeni kuwa watulivu huku mkivuta subra,Serikali yenu ni sikivu na niwahakikishieni tu muda si mrefu mgogoo huu utatatuliwa,"Dkt.Mahenge.

Aidha kuhusu suala la wao kupigwa na baadhi ya Askari wa Pori hilo, Dkt. Mahenge amemuagiza msimamizi Mkuu wa pori hilo Khadija Malongo,kuwaelekeza Askari wake kutowanyanyasa wananchi hao bali wafate sheria na taratibu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages