Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa mara ya kwanza imefanya upasuaji mkubwa wa kuondoa vivimbe katika mishipa ya damu kwenye ubongo (cerebral aneurysms) kwa mgonjwa aliyekywa akisumbuliwa na tatizo hilo.
Kufanyika kwa upasuaji huu ni hatua ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi na kuhakikisha matibabu ya ubingwa wa juu yanatolewa hapa nchini.
Daktari Bingwa mshauri wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu kutoka Korea Kusini, Prof. Huh Seong akifafanua jambo kuhusu upasuaji wa kuondoa vivimbe kwenye ubongo wa Bi Cosila Tambila ambaye amefanyiwa upasuaji huo kulia ni Dkt.Alvin Miranda akifuatiwa na Dk.Raymond Mkaundi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇