Serikali ya awamu ya Tano Chini ya Uongozi wa Dr John Joseph Pombe Magufuli kwa kushirikiana na Sekta binafsi inatekeleza mkakati mahsusi kwa ajili ya kuwajengea ujuzi nguvukazi ya Watanzania ili waweze kushiriki kikamilifu katika Uchumi wa Viwanda.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde wakati wa ziara fupi katika kiwanda cha OpenSanit cha kuzalisha Sare,viatu ( askari na safety boots ), Gum Boots ( boots za Mvua), Mahema,maturubai, na
Mifuko mbadala kilichopo Tabata,Jijini Dar es salaam kinachomilikiwa na Muwekezaji mzawa Kijana Ndg. Octavian Mshiu ambapo Naibu Waziri Mavunde amempongeza muwekezaji huyo kwa kuajiri zaidi ya Vijana 200. “Nakupongeza kwa hatua hii kubwa ya uwekezaji wenye tija sana kwa nchi yetu,Serikali itaendelea kushirikiana nawe katika eneo hili la ukuzaji ujuzi kwa nguvukazi ya Watanzania ili azma ya Serikali ya ifikapo mwaka 2025 asilimia 40 ya nguvukazi kuajiriwa viwandani itimie” amesema Mavunde.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇