LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 24, 2019

MATUMIZI YA SARAFU ZA KIGENI YASITISHWA

Zimbabwe imetangaza leo kuwa itasitisha matumizi ya sarafu za kigeni ambazo zilichukua nafasi ya dola ya Zimbabwe iliyokabiliwa na anguko kubwa kabisa la thamani miaka 10 iliyopita.

Taifa hilo lililo kwenye mgogoro wa kiuchumi linakabiliwa hivi sasa na kupanda kwa bei za bidhaa ambapo takwimu rasmi zinaonesha mfumuko wa bei unafikia asilimia 100.

Benki kuu ya Zimbabwe imesema kwenye taarifa yake, kuwa fedha halali zitakuwa ni noti za hati fungani na sarafu mpya ya RTGS ambazo zilianzishwa baada ya kupungua kwa noti za dola za Marekani.

Tangazo la Benki Kuu limesema, dola ya Marekani, randi ya Afrika Kusini, sarafu nyingine za kigeni na dola ya Zimbabwe hazitotumika kama fedha halali katika malipo yoyote nchini humo.

Serikali ya Zimbabwe imeahidi kuchapisha sarafu mpya za nchi hiyo hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages