Wanasiasa, wafanyabiashara na wawakilishi wa asasi za kiraia wapatao 1,000 wanakutana nchini Jordan leo katika Kongamano la Uchumi Duniani (WEF), kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.
Kongamano hilo la siku mbili, linalofanyika karibu na Bahari Iliyokufa yani Dead Sea, litajadili ukosefu wa ajira, migogoro, maendeleo ya kiuchumi na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo hayo. Mfalme wa Jordan Abdullah ndiye atakaelifungua kongamano hilo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas, Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov wote watahudhuria kongamano hilo.
Mkutano huo umefanyika wakati kunafanyika machafuko ya kijeshi nchini Libya, pamoja na vuguvugu la kudai demokrasia nchini Algeria lilomlazimisha Rais Abdelaziz Bouteflika kung'oka madarakani baada ya kuiongoza nchi hiyo kwa miaka 20.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇