LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 6, 2019

NAIBU WAZIRI TAMISEMI AWATAKA MAAFISA ELIMU NAO WAINGIE DARASANI KUFUNDISHA

Na John Walter-Manyara

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI) anayesimamia sekta ya elimu Mwita Waitara leo April 6.2019 ametoa maagizo kwa maafisa elimu wote nchini kuhakikisha wanasimamia fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya elimu zikafanye kazi husika.

Aidha amewataka maafisa hao kuwa na vipindi vya  kufundisha katika shule zilizopo maeneo yao kwa kuwa hiyo ndio taaluma yao.

Agizo hilo amelitoa leo alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Michezo kwa wanafunzi wa shule za  Sekondari [UMMISETA] ambayo kitaifa mwaka huu wa 2019 yamezinduliwa katika mkoa wa Manyara huku shule 18 za Serikali na binafsi zikijitokeza katika uzinduzi huo katika uwanja wa Kwaraa mjini Babati,na yanatarajiwa kukamilika mwezi june mkoani Mtwara.

Amesema umefika muda sasa masomo ya Michezo mashuleni kuheshimiwa na kupewa kipa umbele na sio kufanywa kama ni kitu cha ziada,kwamba wanafunzi wafundiswe darasani kwenda kwenye viwanja kufanya kwa vitendo.

Michezo hii ya UMMISETA mwaka 2019 imedhaminiwa na Kampuni ya Coca cola ambao wametoa vifaa vya michezo kwa shule zote za Sekondari nchini huku ikiwa na Kauli mbiu  kwa mwaka isemayo”Michezo na Sanaa kwa elimu Bora na Ajira.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages