LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 6, 2019

BENK YA DUNIA YAPATA RAIS MPYA


Bodi ya utendaji ya benki ya dunia imempitisha kwa kauli moja David Malpass kuwa Rais wa 13 wa taasisi hiyo ya fedha.

Bwana Malpass aliyekuwa afisa mwandamizi kwenye wizara ya fedha nchini Marekani ataanza kuutumikia wadhfa huo Jumanne ijayo na hivyo kuchukua nafasi ya bwana Jim Yong aliyejiuzulu miaka mitatu kabla kumalizika kwa muhula wake.

Kuteuliwa kwa bwana Malpass kumesababisha lawama duniani kote kutokana na msimamo wake wa kuikosoa benki ya dunia.

Hata hivyo alipokuwa kwenye wizara ya fedha alisaidia katika juhudi za kupatikana kiasi cha dola bilioni 13 kwa ajili ya kuuongeza mfuko wa benki hiyo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages