LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 14, 2019

UUNGAJI MKONO WA PAMOJA WA WANANCHI WA IRANI KWA JESHI LA WALINZI WA MAPINDUZI SEPAH

Katika maandamano hayo kulitolewa taarifa iliyowataja viongozi wa Marekani kuwa wahusika wa miradi ya kihalifu na watenda jinai wakubwa dhidi ya binaadamu ikiwemo mauaji dhidi ya raia wa Yemen, Nigeria, Bahrain, Palestina, Afghanistan, Syria na Iraq, kama ambavyo serikali ya Washington ni dhihirisho halisi la ugaidi na mlezi wa wimbi hilo la ugaidi duniani. Washiriki wa maandamano hayo, walitoa taarifa ya uungaji mkono wa kila upande kwa serikali ya Iran wakiitaka iendelee kuziunga mkono nchi na mataifa yanayokandamizwa na ubeberu wa Marekani na utawala haramu wa Kizayuni na kwamba suala hilo ni wadhifa wa kidini, mapinduzi ya Kiislamu na wa kibinaadamu pia. Itakumbukwa kuwa tarehe nane ya mwezi huu serikali ya Marekani sambamba na kuchukua hatua iliyo kinyume na sheria zote za kimataifa na katika kulivunjia heshima taifa la Iran, ililiweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH katika orodha inayoitwa kwa istilahi ya kigaidi.

Mamilioni ya Wairan wakiandamana Ijumaa iliyopita kuliunga mkono jeshi la SEPAH

Hata kama hatua hiyo haina thamani yoyote ya kijeshi wala ya kisiasa, kama ambavyo pia haina uhalali wowote wa kisheria, pamoja na hayo inahesabiwa kuwa ni harakati moja ya kijeuri na inayokiuka wazi sheria, iliyofanywa na serikali ya Marekani. Aidha hatua hiyo itapelekea kuzuka matukio yasiyotarajiwa kwa usalama na amani ya eneo la Asia Magharibi na dunia kwa ujumla. Kwa mtazamo wa weledi wa mambo, siasa za Marekani katika kuliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH katika orodha ya makundi ya kigaidi, kabla hazijaleta changamoto kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, zimeiletea changamoto kubwa Washington yenyewe. Katika uwanja huo, jarida la Kimarekani la Foreign Policy sambamba na kukiri uwezo mkubwa usio na mbadala wa Jeshi la Ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, limeandika: "Kama Iran itaamua kuchukua hatua zake za kijeshi, itaweza kuwazidishia matatizo makubwa askari wa Marekani. Hii ni kwa kuwa Iran ndio yenye machaguo mengi zaidi katika uwanja huo."Itafaa kuashiria kuwa, hiyo si hatua ya kwanza kwa Marekani kuiweka taasisi rasmi ya serikali ya nchi mojawapo katika orodha hiyo ya kigaidi.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, ambalo limefelisha sana njama chafu za Marekani, Israel Saudia nk

Viongozi wa serikali ya Washington wanadai kwamba kitendo hicho kina lengo la kuzidisha chuki kwa mashirika ya kigeni ili kwa njia hiyo yasiweze kufanya biashara na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hata hivyo weledi wa mambo wanaofuatilia hali ya eneo la Mashariki ya Kati, wanafahamu kwamba madai hayo ni aina mojawapo ya propaganda chafu dhidi ya nchi hii. Ukweli ni kwamba hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani katika kuliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, imekiuka wazi misingi ya utawala wa sheria na hati za kimataifa, ikiwemo sheria ya usawa wa kujitawala nchi za dunia, na kwa hiyo, harakati hiyo ya White House itapelekea kushadidisha mizozo katika ngazi ya makabiliano yasiyoweza kuzuilika. Katika uwanja huo Kioumars Heydari, Kamanda wa Vikosi vya Ardhini vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akiwahutubia Waislamu kabla ya hotuba ya swala ya Ijumaa iliyopita mjini Tehran, ikiwa ni katika kutoa radiamali kufuatia hatua hiyo chafu ya Marekani dhidi ya jeshi la SEPAH la nchi hii alisema: "Ninawatangazia Marekani, utawala haramu wa Kizayuni na muungano wa Kiebrania (yaani muungano wa kijeshi wa nchi za Kiarabu) kwamba, hatua ya Trump dhidi ya jeshi la SEPAH ni ya kijinga sana ambayo itawaweka hatarini daima askari wa Kimarekani katika maeneo mbalimbali ya dunia hususan askari wa nchi hiyo walioko eneo la Asia Magharibi (CENTCOM)."

Sehemu ndogo ya nguvu za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH

Kama alivyosema Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mohammad Javad Zarif katika barua aliyomtumia AntĂłnio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la umoja huo katika kulalamikia hatua hiyo chafu ya Marekani kwamba: "Kamandi ya askari wa Kimarekani ilioko katika eneo la Asia Magharbi (CENTCOM) ni mbeba dhima ya jinai mbalimbali za kigaidi katika eneo hilo....." Ni kwa ajili hiyo ndio maana Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuzingatia historia mbaya ya askari wa Kimarekani katika eneo la Asia Magharibi hasa katika kuwaunga mkono magaidi, likaiweka kamandi hiyo ya jeshi la Marekani katika orodha ya makundi ya kigaidi. Hivyo kwa vyovyote iwavyo, Marekani ndiye muhusika na mbeba dhima wa kile kitakachotokea katika eneo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages