LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 14, 2019

MAJAJI WA ALGERIA KUSUSIA UCHAGUZI MKUU UJAO WA JULAI

Idara ya Mahakama nchini humo imesema majaji wa nchi hiyo hawatashiriki uchaguzi wa rais, wakisisitiza kuwa watasimama na watu walioandamana wakitaka mabadiliko.
Mawakili na watetezi wa haki za binadamu nchini humo wameliunga mkono tangazo hilo la majaji, wakisisitiza kuwa majaji hao hawapaswi kuwa chini ya mashinikizo ya mtu au taasisi yoyote.
Rais wa muda wa Algeria, Abdelkader Bensalah alitangaza hivi karibuni kuwa, tarehe 4 Julai mwaka huu ndiyo siku ya kufanyika uchaguzi wa kumtafuta mrithi wa Abdelaziz Bouteflika, rais wa nchi hiyo aliyejiuzulu.
Rais wa muda wa Algeria, Abdelkader Bensalah
Bensalah anashikilia wadhifa huo wa rais wa muda wa Algeria kwa muda wa siku 90. 
Kufuatia maandamano makubwa ya upinzani ya kupinga serikali yaliyofanyika kwa muda wa wiki sita nchini Algeria, hatimaye tarehe 2 Aprili Abdelaziz Bouteflika alitangaza rasmi uamuzi wa kujiuzulu wadhifa wa urais baada ya kuweko madarakani kwa kipindi cha miaka 20

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages