LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 14, 2019

WAANDAMANAJI WA SUDAN WAWASILISHA MADAI KWA BARAZA LA KIJESHI

Waandaaji wa maandamano ya nchini Sudan hapo jana wamewasilisha madai yao ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa Serikali ya kiraia walipokutana na viongozi wapya wa kijeshi nchini humo.

Maelfu ya waandamanaji wengine walibakia nje ya makao makuu ya jeshi katika Mji Mkuu wa Khartoum, wakiendeleza shinikizo kwa baraza la kijeshi la mpito lilochukua madaraka ya nchi baada ya kuondolewa Rais wa muda mrefu Omar al-Bashir Alhamisi iliyopita.

Ujumbe wa watu 10 uliwasilisha madai hayo ya waandamanaji mbele ya baraza hilo la kijeshi, Moja ya madai yao ni kufanyia mageuzi idara ya usalama wa taifa inayoogopwa, ambayo mkuu wake Salih Ghosh amejiuzulu kufuatia kuondolewa madarakani rais Bashir.

Mapema jana Mkuu mpya wa Baraza la Kijeshi la Mpito Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ameahidi kuuondoa utawala la Bashir na amefuta marufuku ya kutoka nje usiku. Waandamanaji hata hivyo wameapa kuendelea na maandamano hadi pale baraza hilo la kijeshi litakapopokea madai yao.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages