Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF umetangaza kuwa, maelfu ya watoto wa Sudan Kusini wangali wanatangatanga na hawajaungana na familia zao.
Taarifa ya Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF imeeleza kuwa, takribani watoto 6,000 wa Sudan Kusini wangali wakimbizi na hawajafanikiwa kuungana na familia zao ikiwa ni miaka kadhaa sasa tangu wapoteana na familia zao baada ya kuzuka vita katika nchi hiyo changa zaidi barani Afrika.
Ni miaka mitano sasa imepita tangu vita vilipozuka huko Sudan Kusini ambapo raia milioni nne wa nchi hiyo wamelazimika kuwa wakimbizi hasa katika nchi jirani ya Uganda.
Ripoti ya Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF inabainisha kuwa, watoto 8,000 wa Sudan Kusini hadi sasa hawajafanikiwa kuungana na familia tangu walipotengana na ndugu zao miakka kadhaa iliyopita.
Kadhalika Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF umeonya kuwa, watoto wakimbizi wa Sudan Kusini waliopoteana na familia zao wamo katika hatari kuingizwa
katika vitendo vya utumiaji mabavu, miamala mibaya na hata kutumiwa vibaya.
Nchi ya Sudan Kusini iliyojitenga na Sudan mwaka 2011 kwa uchochezi wa nchi za Magharibi hususan Marekani, Disemba mwaka 2013 ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na mamilioni ya wengine kulazimika kuwa wakimbizi. Mapatano ya amani baina ya mahasimu nchini humo yamefikiwa hivi karibuni lakini bado yanalegalega
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇