LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 6, 2019

TRUMP: MAREKANI IMEJAA HADI POMONI, HATUWEZI KUPOKEA WATU WENGINE

Trump aliyasema hayo jana Ijumaa, wakati akiongea na waandishi wa habari katika eneo la Calexico jimboni California, mpakani mwa nchi hiyo na Mexico.
Trump ambaye amekuwa akishinikiza kujengwa ukuta wa kibaguzi katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico amesema, "Kuna hatari katika mpaka wa kusini. Hatuwezi kukupokeeni. Hatuwezi kuendelea kukupokeeni, nchi yetu imejaa, kwa hiyo geukeni mrejee mlikitoka."
Japokuwa takwa la Trump la kutengewa dola bilioni tano na milioni 700 zinazohitajika kwa ajili ya ujenzi wa ukuta huo bado halijatimizwa, lakini hivi karibuni kiongozi huyo alilegeza msimamo na kukubali kuendeleza kwa muda shughuli za serikali zilizosita kwa muda wa siku 35 kutokana na vuta nikuvute kati ya yake na Kongresi, juu ya ujenzi wa ukuta huo. 
Mpaka wa Marekani na Mexico
Mwishoni mwa mwaka jana, Trump alionya kuwa, maelfu ya wanajeshi wa nchi hiyo waliotumwa katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico huenda wakalazimika kuwapiga risasi wahajiri wanaotoka katika nchi za Amerika ya Kati na wanaotaka kuingia Marekani kupitia mpaka huo.
Wataalamu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamekosoa kitendo cha Marekani cha kuendelea kuwazuilia wahamiaji na raia wa kigeni wanaotafuta hifadhi nchini humo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages