LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 6, 2019

MALAYSIA: MASHINIKIZO HAYATATULAZIMISHA KUJIUNGA NA ICC

Waziri Mkuu wa Malaysia amesema mashinikizo hayataifanya nchi hiyo ijiunge na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
Mahathir Mohammad aliyasema hayo jana Ijumaa katika kikao na waandishi wa habari mjini Putrajaya na kuongeza kuwa, mashinikizo yanayotolewa na wapinzani katu hayatalifanya taifa hilo lisaini Mkataba wa Roma uliounda makahama hiyo iliyoko mjini The Hague nchini Uholanzi.
Dakta Mahathir Mohammad amesema jambo ambalo linaifanya nchi hiyo isijiunge na ICC ni kutokana na chombo hicho kukabiliwa na 'mkanganyiko wa kisiasa' uliosababishwa na watu wenye ajenda binafsi. 
ICC iliyounda mwaka 2002, inahesabiwa kuwa ni ya kwanza ya kudumu inayoshughulikia jinai za vita duniani.
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC)
Utendaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai za Kivita umekuwa ukikosolewa, huku taasisi hiyo ikitakiwa kujiepusha na vigezo vya undumakuwili na ubaguzi katika kushughulikia kesi za jinai.
Marekani, Russia na China ni miongoni mwa nchi zilizokataa kusaini Mkataba wa Roma, huku nchi kadhaa kama Burundi na Ufilipino zikijiondoa kwenye mahakama hiyo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages