LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 6, 2019

IRAN NA RUSSIA; UDHARURA WA KUSHIRIKIANA KATIKA UGA WA HABARI

Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB), ambaye amefanya safari katika mji mkuu wa Russia, Moscow, amesema katika mazungumzo yake na Alexey Nikolov, Mkurugenzi Mwendeshaji wa kanali ya televisheni ya Russia Today kwamba, kupanuliwa ushirikiano katika sekta ya habari baina ya Iran na Russia ni hatua muhimu.
Aidha amebainisha kuwa, hatua hiyo ni muhimu mno katika njia ya kuhitimisha ubeberu na ukiritimba wa madola ya Magharibi katika tasniaMkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB), ya habari.Katika mazungumzo yake hayo hapo jana Ijumaa, Dakta Peyman Jebelli ameashiria kufungwa kwa akaunti za Twitter na kurasa za mitandao ya kijamii ya Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) katika Facebook na akasisitiza kwamba: Kwa kuzingatia kuwa hatua zinazofanana na hizo zimechukuliwa dhidi ya vyombo vya habari vya Russia pia, Tehran na Moscow zinaweza kuimarisha ushirikiano wao wa vyombo vya habari ili kukabiliana na hatua hizo.
Kwa upande wake, Alexey Nikolov, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Russia Today, naye pia amekosoa vikali miamala ya kindumakuwili ya Marekani na Ulaya kuhusiana na kadhia ya uhuru wa maoni na vyombo vya habari na akabainisha kwamba, nchi za Magharibi zina kaulimbiu za maneno matamu kuhusu uhuru wa maoni na vyombo vya habari, lakini kwa masikitiko ni kwamba, katika vitendo zinatumia nguvu zao zote kuzima sauti za wapinzani na vyombo huru vya habari.
Katika ulimwengu mpana wa mawasiliano, vyombo vya habari vya Magharibi vimekuwa vikifanya kila viwezalo katika nukta yoyote ile ya dunia kuhodhi sekta ya habari. Katika hali ambayo, vyombo vya habari vya Magharibi vimekuwa vikitangaza habari nyingi zilizojaa propaganda kubwa kwa ajili ya kupotosha ukweli wa mambo, mwenendo huo mchafu umelifanya suala la kuongezwa kiwango cha ushirikiano wa habari kwa ajili ya kukabiliana na harakati hii ya upande mmoja kuwa na udharura maradufu. 
Dakta Peyman Jebelli, Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB), katika mazungumzo yake na lexey Nikolov, Mkurugenzi Mwendeshaji wa kanali ya televisheni ya Russia Today
Wataalamu wa sekta ya habari wanaamini kuwa, ili kuinua kiwango cha uelewa na ufahamu katika ulimwengu na kufikiwa malengo ya ufikishaji habari kwa uhuru kamili na kufungamana na msingi wa uhuru wa kutoa maoni, kuna haja ya kuweko mtazamo mmoja baina ya mashirika huru ya habari ambayo yanafanya kazi kwa kuheshimu misingi ya tasnia hii. Katika uga huu, Iran na Russia zinaweza kuwa na nafasi muhimu mno. Ushirikiano katika uga wa habari baina ya Iran na Russia na kutolewa uchambuzi wa wazi, wa kina na unaoakisi ukweli wa mambo kuhusiana na matukio mbalimbali ni jambo ambalo linaweza kuwafanya walengwa wapate habari za kweli na za uhakika.
Katika uwanja huu, Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limefanya ubunifu wenye utendaji mzuri katika uga wa kimataifa na kwa kutoa mitazamo mipya kupitia majimui ya redio na televisheni katika kanali zenye watazamaji na wasikilizaji wengi wa kitengo cha matangazo ya ng'ambo kama Press TV, al-Alam, Parstoday na Iran Press limeweza kupiga hatua muhimu na athirifu na kufanikiwa kukabiliana na mashinikizo ya vyombo vya habari vya madola ya Magharibi.
Filihali, vyombo vya habari vya Iran na Russia vina uwezo unaonasibiana na uhusiano wa kisiasa wa nchi mbili hizi na hivyo vinaweza kufanya juhudi za pamoja na kuinua kiwango cha ushirikiano huu. Katika uwanja huu, kanali ya televisheni ya Russia Today na Press TV pamoja na kanali nyingine za matangazo ya ng'ambo za Iran zina ushirikiano mzuri na bila shaka ushirikiano huu unaweza kupanuliwa katika nyuga tofauti zikiwemo za mabadilishano ya tajiriba na uzoefu, utoaji mafunzo na zana za kiufundi.
Dakta Peyman Jebelli, Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akiwa nchini Russia
Talaei-Nik, mchambuzi wa masuala ya kisiasa katika uga wa vyombo vya habari anasema kuwa, mkakati mkuu wa kusambaratisha vita vya vyombo vya habari vya Magharibi ni kuimarishwa harakati za kihabari za Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuzalishwa vipindi kwa ushirikiano na vyombo huru vya habari. Mchambuzi huyu anaamini kuwa, ushirikiano huu unaweza kwa kiwango fulani kujaza pengo la upashaji habari na kuakisi matukio kwa ukweli na uhakika wake.
Hapana shaka kuwa, kusukuma mbele gurudumu la malengo haya kunahitajia kuandaa uwezo mpya katika fremu ya suhula na ushirikiano wa kihabari na kuzalisha vipindi kwa ushirikiano sambamba na kuwatumia wataalamu na watu wenye vipawa katika uga wa habari. Hivi sasa tunashuhudia kufunguliwa ukurasa mpya wa ushirikiano wa sekta ya habari baina ya Iran na Russia katika safari ya Peyman Jebeli, Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) huko Moscow Russia.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages