Katika kukaribia uchaguzi wa kabla ya wakati wa bunge ndani ya utawala haramu wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo, amepatwa na wasi wasi mkubwa kufuatia kutangazwa matokeo ya uchunguzi wa maoni kuhusiana na uchaguzi huo.
Uchaguzi wa 21 wa bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel, utafanyika Jumanne ya kesho. Uchaguzi huo ulikuwa umepangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu, hata hivyo tofauti zilizoibuka ndani ya baraza la mawaziri na pia kitendo cha baadhi ya viongozi wa baraza hilo kujiondoa ndani ya serikali ya Netanyahu, zilipelekea kusambaratika kwa baraza hilo sambamba na kuibuka udharura wa kuitishwa kwa uchaguzi huo wa mapema. Dhana ya Netanyahu katika kutoa amri ya kufanyika uchaguzi huo wa kabla ya wakati, ilikuwa kwamba ushindi wake mwepesi katika uchaguzi huo, utaweza kuimarisha nafasi yake ya kisiasa na hivyo kumwezesha kuunda baraza jipya na lenye maelewano zaidi. Hata hivyo pamoja na hayo, taarifa za hivi karibuni ,hasa ikiwa imesalia siku moja kabla ya kufanyika uchaguzi, zinaonyesha kwamba mahesabu ya Netanyahu hayakuwa sahihi, kwani mrengo wa kulia na chama cha Likud hauko katika mazingira mwafaka ya kuweza kukabiliana na wapinzani wake. Katika uwanja huo, matokeo ya kura ya maoni ukiwemo uchunguzi wa kanali ya 13 ya utawala huo yanaonyesha kwamba muungano wa ‘Buluu na Nyeupe’ ambao unawakutanisha pamoja majenerali wa Israel na unaoongozwa na Benny Gantz, Mkuu wa zamani wa Majeshi ndani ya utawala huo, utapata ushindi wa viti 36 kati ya viti 120 vya bunge na baada ya hapo chama cha Likud kitapata ushindi wa viti 30.
Iwapo matokeo ya uchaguzi yataenda sawa na uchunguzi huo, basi Netanyahu na mirengo ya kulia watakuwa wameshindwa vibaya kwenye uchaguzi huo. Ni kwa ajili hiyo, ndio maana Netanyahu sambamba na kuonyesha wasi wasi wake mkubwa kufuatia matokeo hayo ya uchunguzi wa maoni akasema: "Chama cha mrengo wa kulia kiko hatarini kupoteza uongozi katika uchaguzi wa bunge wa tarehe 9 Aprili." Ukweli ni kwamba kuna sababu mbili zinazotajwa kudhoofika nafasi ya kisiasa ya Benjamin Netanyahu ndani ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Mosi ni mafaili manne ya ufisadi yanayomkabili yeye pamoja na mke wake. Inafaa kuashiria kuwa, suala la ufisadi unaohusishwa na Benjamin Netanyahu ni lenye historia ndefu ndani ya Israel. Hii ni kusema kuwa, hadi sasa Waziri Mkuu huyo wa Utawala katili wa Kizayuni anahusishwa na mafaili manne ya ufisadi wa fedha, kupokea rushwa, kutumia vibaya madaraka, ambapo katika faili la kutumia vibaya madaraka linaihusu pia familia yake akiwemo mke wake Sara Netanyahu. Washindani na wakosoaji wa Netanyahu hususan katika kipindi cha kampeni za uchaguzi walikuwa wakilielezea suala hilo. Pili ni kwamba washindani wa Netanyahu katika mrengo wa kushoto wanatumia mwanya ulioibuka ndani ya mrengo wa kulia. Katika uwanja huo Benny Gantz, mkuu wa zamani wa majeshi ya Israel ambaye anaviongoza vyama vya mirengo yote ya kushoto, ameunda chama kipya alichokipa jina la 'Usalama kwa ajili ya Israel' na kisha kuungana na Yair Lapid, mkuu wa chama cha 'Yesh Atid', pamoja na Moshe Ya'alon na Gabi Ashkenazi makamanda wawili wa zamani wa jeshi la utawala huo haramu wa Kizayuni. Muungano huo wa makamanda wa zamani wa jeshi la Israel umezalisha muungano unaoitwa 'Buluu na Nyeupe' kwa ajili ya kujitosa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi huo wa kesho.
Hii ni katika hali ambayo, mirengo ya kulia inayoundwa na Naftali Bennett na Ayelet Shaked, bado inaendelea kushuhudia mpasuko. Nukta muhimu ni hii kwamba washindani wa Netanyahu ndani ya mrengo wa kulia si tu kwamba hawaamini kuwa Netanyahu hana mshindani ndani ya muungano huo, bali wanaamini kwamba utawala wake wa kipindi cha miaka 13, umesababisha kuongezeka zigo la ufisadi kwake na kwa familia yake na matokeo yake ni kutoa pigo kubwa kwa mirengo ya kulia ndani ya Israel. Alaakullihal, uchaguzi wa kesho utaainisha mustakbali wa uongozi ndani ya utawala huo haramu. Hata hivyo Benjamin Netanyahu ametahadharisha juu ya hatari inayoukabili mrengo wa kulia, na hakuna shaka kwamba wasi wasi wake huo unahusu hatma yake mbaya baada ya kushindwa kwenye uchaguzi huo.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇