LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 8, 2019

UN YAANZISHA UTARATIBU WA KIBENK WA UFIKISHAJI MISAADA YA FEDHA TASLIMU KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO IRAN

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Iran amesema: Umoja wa Mataifa umeanzisha utaratibu maalumu wa kibenki kwa ajili ya kufikisha misaada ya fedha taslimu kwa waathirika wa mafuriko nchini Iran.
Ugochi Daniels ameyasema hayo leo pembeni ya warsha ya wawakilishi wa ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko hapa nchini iliyofanyika mjini Tehran kuzungumzia utaratibu wa ufikishaji misaada katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko. Daniels amewaeleza waandishi wa habari kuwa: Mbali na kuanzisha utaratibu wa kibenki kwa ajili ya kufikisha misaada ya fedha taslimu kwa ajili ya waathiriwa wa mafuriko nchini Iran, Umoja wa Mataifa umetoa msaada pia wa dola 1,420,000 za ununuzi wa vifaa vya tiba na afya, maji, suhula za kiafya pamoja na kuwapatia hifadhi watu walioathiriwa na mafuriko.
Alipoulizwa kuhusu kimya cha Umoja wa Mataifa kuhusiana na mwenendo wa kiuadui wa Marekani wa kuzuia kufikishwa misaada kwa wananchi wa Iran walioathiriwa na mafuriko, mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa hapa nchini amesema: Vikwazo vya Marekani si vya kiadilifu.
Baadhi ya maeneo ya Iran yaliyoathiriwa na mafuriko
Daniels amebainisha kwamba: Jitihada kadhaa zimefanywa katika ngazi ya juu kabisa ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya ufikishaji misaada kwa waathirika wa mafuriko na kuhakikisha misaada hiyo haizuiliwi kufikishwa nchini.
Baada ya kutokea janga la mafuriko katika baadhi ya maeneo ya kaskazini, magharibi na kusini mwa Iran, Marekani ilichukua hatua ya kuzifunga akaunti za fedha zenye mfungamano na shirika la Hilali Nyekundu la Iran ili kuvuruga shughuli za ufikishaji misaada za shirika la Msalaba Mwekundu na nchi zingine duniani kwa ajili ya watu walioathirika na mafuriko hapa nchini.
Idara ya uchunguzi wa vifo nchini Iran imetangaza kuwa jumla ya watu 70 wamefariki dunia kutokana na mafuriko katika maeneo tofauti nchini.../

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages