LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 13, 2019

RAIS MAGUFULI AMTUNUKU LUTENI KANALI KUWA BRIGEDIA JENERALI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amempandisha cheo aliyekuwa Luteni Kanali, Charles Mbuge kuwa Brigedia Jenerali baada ya kufurahishwa na utendaji wake wa kazi katika kusimamia ujenzi wa miradi mbalimbali ya serikali ikiwemo ujenzi wa ukuta wa Mererani.

"Ninawapongeza maofisa walioshiriki kukamilisha mradi huu na Kanali Mbuge alisimamia ujenzi wa majengo mbalimbali ya serikali pamoja na ukuta wa Mererani hivyo kuanzia leo atakuwa Brigedia Jerenali sitaki kuchelewa hivyo ninataka CDF ukafanye utaratibu wa vile vinavyotakiwa kuwekwa kwenye mabega awekewe,” amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo hatua za haraka za kukamilisha kumtunuku cheo kwa nafasi hiyo ya Brigedia vikafanyika mbele ya Rais Magufuli.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages