LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 13, 2019

RAIS MAGUFULI: AMBAYE OFISI YAKE HAITAKAMILIKA, KAMA UTAKUWEPO MWEMBE IWE NDIO OFISI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa suala la kuhamia Dodoma sio kazi rahisi hivyo viongozi ambao hawajakamilisha ujenzi kama kutakuwepo na Muembe ndio itakuwa ofisi yao ili wananchi wakienda wawakute.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali jijini Dodoma.

"Kuhamia Dodoma sio kazi rahisi, wakati Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wanahamia niliuliza Wizara zitahamia lini kila mtu alijibu lake, nilitoa maagizo ndani ya miezi 3, nyumba ziwe zimemalizika ambaye hatamaliza kama kutakuwepo na mwembe ndiyo uwe ofisi yake.

Aidha, Rais Magufuli aliongeza kuwa " Kuanzia Jumatatu Serikali yote iwe huku, ili wananchi wanaokuja kwenye shida waje Dodoma, tusipoamua hivi tutabaki na majengo huku ofisi zitakuwa Mkoani."

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages