Benjamin "Benny" Gantz ni mkuu wa zamani wa jeshi la Israeli anayeamini kwamba anaweza kumng'oa waziri mkuu Benjamin Netanyahu katika uchaguzi mkuu unaofanyika.
Ni mwanzo Luteni Jenerali huyo aliyestaafu mwenye umri wa miaka 59 anajitosa katika siasa na kuahidi kuliunganisha taifa ambalo "lilikuwa limepotea njia".
Gantz alizaliwa Kfar Ahim mnamo 1959, kijiji cha wakulima kilichopo Israel ya kati kilichoundwa na wahamiaji.
Babake na Mamake Nahum na Malka ni manusura wa mauaji ya halaiki ya wayahudi.Akiwa kijana Gantz alisomea katika shule ya bweni katika kijijij cha vijana karibu na Tel Aviv.
Baada ya kumaliza shule huko mnamo 1977, alijisajili katika kikosi cha ulinzi wa Israel (IDF. Jukumu lake la kwanza lilikuwa na kumlinda rais wa Misri Anwar Sadat alipokuwa katika ziara ya historia nchini Israel.
Mwanajeshi wa mwisho kuondoka Lebanon
Miaka miwili iliyopita, alifuzu kutoka shule ya IDF na kupewa wadhifa wa kamanda katika kikosi wanajeshi wa angani. Baada ya hapo alikwea katika nyadhifa mbali mbali.
Amekuwa na majukumu makuu katika kampeni za kijeshi ikiwemo mnamo Mei 1991 alipokiongoza kikosi maalum cha makomando Israeli katika operesheni ya kuwasafirisha maelfu ya wayahudi wa Kiethiopia kwenda Israel katika muda wa siku moja na nusu.
Kama mkuu wa kikosi cha Judea ndani ya IDF mnamo 1994, alikuwa na jukumu la kurudisha usalama katika mji uliogawanayika wa Hebron, katika eneo lililokaliwa la ukingo wa magharibi, baada ya mkaazi wa kiyahudi kuwaua raia 29 wa Palestina katika shambulio lililotekelezwa kwenye eneo tukufu la makaburi na mskiti wa Ibrahimi.
Katikati ya muda aliyohudumu katika jeshi, alikaa mwaka mmoja nchini Marekani mnamo 1997 na kupata shahada ya uzamifu katika usimamizi wa rasilmali za kitaifa kutoka chuo kikuu cha ulinzi wa taifa.
Kufikia 1999, alikuwa afisa mkuu nchini Israeli aliyepo katika enoe lililokaliwa la Lebanon kusini - nafasi aliyoipokea baada ya mtangulizi wake kuuawa katika mlipuko wa bomu liliotegwa barabarani. Jenerali Gantz amesema alikuwa mwanajeshi wa mwisho kuvuka mpaka na kufunga rasmi lango kuu mpakani wakati wa najeshi wa Israeli walipoondoka nchini Lebanon mnamo 2000.
Operesheni Gaza
Mwaka uo huo, aliteuliwa kuwa kamanda wa kitengo cha Judea na Samaria. Alianza kazi siku chache tu kabla ya shambulio la pili la intifada, au vuguvuug la raia wa Palestina linalopinga uvamizi wa Israeli.
Aliwahi pia kuwa kamanda wa jeshi la nchi kavu la IDF katika vita vya mnamo 2006 huku kukiwepo vuguvugu la waasi la Hezbollah Lebanon - mzozo ambao jeshi la Israeli na viongozi wa serikali walishutumiwa pakubwa.
Kufikia mwisho wa 2007 aliondoka Israel kwenda Marekani kuhudumu kama mjumbe wa kijeshi huko Washington DC - nafasi aliyohudumu kwa miaka miwili , kabla ya kuitwa kurudi Israel kuhudumu kama naibu mkuu wa jeshi la ulinzi nchini IDF.
Mwaka 2011, akawa mkuu wa 20 wa majeshi nchini kwa ghafla baad aya kuibuka mzozo kati ya waziri wa ulinzi Ehud Barak na mkuu wa majeshi aliyekuwa anaondoka Jenerali Gabi Ashkenazi, kuhusu wagombea na kufutiliwa mbali kwa mgombea mkuu.
Katika muda wake huo jeshi liliidhinisha operesheni mbili kuu mnamo 2012 na 2014 dhidi ya wanamgambo wa Palestina huko Gaza,walioongozwana kundi la Hamas, ambalo viongozi wa Israeli walisema yalinuiwa kusitisha mashambulio dhidi ya raia wake.
Maafisa wa Palestina na makundi ya kutetea haki za binaadamu wamelishutumua jeshi la Israeli kwa uhalifu wa kivita wakati wa mzozo huo.
Lakini Gantz alisema vikosi vyake viliwajibika kuzuia vifo vya raia na kulilaumua Hamas kwa kuweka miundo mbinu ya kijeshi katika makaazi ya watu.
Mismamizi mkuu wa fedha Israel baadaye alimshutumu Gantz na viongozi wengine katika jeshi na serikali kwa kushindwa kujitayarisha ipasavyo kwa tishio la njia nyingi za chini kwa chini zilizochimbwa na kundi la Hamas walizotumia kutekeleza mashambulio wakati wa vita.
Kabla ya kumalizika kwa hatamu ya kijeshi ya Gantz mnamo 2015, Benjamin Netanyahu alimsifu kwa miongo kadhaa "ya huduma maridhawa" na kumtaja kuwa "wa kiwango cha juu, aliye muadilifu , muajibikaji na kiongozi mwenye busara".
Lakini miaka minne baadaye, Netanyahu kamwe hakutoa sifa tena kwa mwanamume aliyegeuka kuwa mpinzani wake mkuu kwa wadhifa huo mkuu, na badala yake kumtaja kuwa mtu "dhaifu wa mrego wa kushoto".
Wanajeshi wakongwe waungana nguvu
Gantz ametangaza kwamba iwapo chama chake cha Israel Resilience party kitashinda katika uchaguzi mkuu, ataunda serikali itakayo "chukua hatua kwa uwajibikaji, kwa uamuzi mmoja na madhubuti".
Ametoa matamshi makali kuhusu Iran na kumuonya kiongozi wa Hamas huko Gaza, Yehiya Sinwar, "usinijaribu tena". lakini ameahidi pia "kushinikiza amani" na " kutopoteza nafasi ya kuleta mageuzi kieneo".
Ameisistiza pia kwamba "fikra ya kwamba waziri mkuu wa Israel anaweza kusalia madarakani wakati anakabiliwana mashtaka inastaajabisha " - akigusia tangazo la mkuu wa sheria mnamo Februari kwamba anapanga kumshtaki Netanyahu kwa makosa ya rushwa, kukisubiria kusikizwa kesi.
Katika uchaguzi huu, chama cha Israel Resilience kimeunda muungano unaoitwa Blue and White - samawati na nyeupe, rangi za bendera ya taifa - pamoja na chama cha Yesh Atid cha mrengo wa wastani cha aliyekuwa waziri wa fedha Yair Lapid.
Gantz na Lapid wamekubaliana kuchukua hatamu za kupokezana kama waziir mkuu iwapo muungano wao utaunda serikali, huku Jenerali huyo wa zamani akishikilia wadhifa huo kwa miaka miwili unusu ya kwanza.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇