Wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART) umesema mlundikano wa abiria katika vituo umetokana na tatizo la uhaba wa mabasi unaosababishwa na baadhi kuharibika na kuhitaji matengenezo hali inayochangia usumbufu kwa wananchi wanaotumia usafiri huo.
Akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kupokea ujumbe wa bodi ya jiji la Kisumu kutoka nchini Kenya unaotembelea mradi huo kwa ajili ya kujifunza, Kaimu mtendaji mkuu Mhandisi Ogare amesema mradi huo ulianza na mabasi 140 na mengine hayafanyi kazi kutokana na ubovu na serikali iko katika mpango wa kutafuta mwekezaji mwengine pamoja na mabasi mapya ili kukabiliana na tatizo hilo.
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa bodi ya jiji la Kisumu toka Kenya wamesema zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wa jiji hilo wanatumia usafiri wa jumuiya na kusababisha mlundikano wa daladala na bodaboda na kuchangia kukwama kwa shughuli za kiuchumi kutokana na utumia muda mrefu barabarani.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇