Askari usalama wa Misri wamewatia nguvuni mamia ya vijana waliofanya maandamano katika maneo mbalimbali ya nchi hiyo wakipinga utawala wa Rais Abdel Fattah al Sisi wa nchi hiyo.
Maandamano hayo yamefanyika baada ya ajali iliyotokea katika kituo kikuu cha treni mjini Cairo na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 20.
Maandamano hayo ya kupinga utawala wa Abdel Fattah al Sisi yalishuhudiwa katika miji ya Qairo, Beheira, Alexandria, Menoufia na Faiyum.
Mjini Cairo waandamanaji walikusanyika mbele ya Msikiti wa al Fat'h wakiwa na mabango yenye maandishi yanayomtaka al Sisi aondoke madarakani. Waandamanaji wengine pia walikusanyika mbele ya msikiti wa al Rahman na kukabiliana na askari usalama waliotia nguvuni makumi ya vijana wakiwemo wasichana kadhaa.
Baada ya ajali ya Jumatano iliyopita iliyosababisha vifo vya makumi ya watu katika kituo kikuu cha treni mjini Cairo, wanaharakati wa masuala ya kisiasa na kijamii walitoa wito wa kufanyika maandamano ya kumtaka Rais Abdel Fattah al Sisi aondoke madarakani.
Wakati huo huo shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetangaza kuwa, ukandamizaji unaofanywa na serikali ya Abdel Fattah al Sisi dhidi ya wanaharakati wa masuala ya kijamii ukiwemo uhuru wa kujieleza nchini Misri ni mkubwa zaidi kuliko ule ulioshuhudiwa katika kipindi cha dikteta wa zamani wa nchi hiyo, Hosni Mubarak.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇