Mwanachama wa Bunge la Seneti na mgombea urais katika uchaguzi wa 2020 nchini Marekani, Elizabeth Warren sambamba na kuyatetea mapatano ya nyuklia ya Iran maarufu kama JCPOA amesema kuwa, hatua ya Washington kujiondoa katika mapatano hayo haikuwa na maana.
Warren aliyeyasema hayo katika kikao cha kusailiwa kamati ya majeshi ya ulinzi ya Marekani katika bunge la seneti na kuongeza kwamba, hatua ya upande mmoja ya Trump ya kujiondoa katika mapatano hayo na kisha kurejesha vikwazo dhidi ya Iran, ilikuwa ya uvurugaji, kwani mwezi uliopita, Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) lilitangaza kwamba Tehran imefungamana na mapatano hayo. Seneta huyo wa chama cha Democrat ameongeza kwamba kuiondoa Marekani katika mapatano hayo bila ya kuwa na mpango mbadala, ilikuwa haina maana yoyote.
Kwa mujibu wa Elizabeth Warren mapatano hayo ya nyuklia ya JCPOA yanaizuia Iran kuweza kuwa na silaha za nyuklia na ameongeza kwamba kuwepo mapatano hayo ni bora zaidi kuliko kutokuwepo. Trump alichukua hatua ya upande mmoja ya kuiondoa nchi yake katika mapatano ya JCPOA hapo tarehe nane Mei mwaka jana na kisha akarejesha vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hatua hiyo ya Trump na ambayo ilitokana na kuchochewa na lobi ya Kizayuni hadi hivi sasa inaendelea kulaaniwa vikali ndani na nje ya Marekani.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇