LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 6, 2019

MAANDAMANO YASHIKA KASI ALGERIA, JESHI LAAPA KUZUIA UMWAGIKAJI DAMU

Maelfu ya wananchi wa Algeria Jumanne waliendeleza maandamano katika mji mkuu Algiers, wakimtaka Rais Abdelaziz Bouteflika aondoke madarakani huku jeshi nalo likiapa kuzuia umwagikaji damu nchini humo.
Maandamano ya Juamnne pia yameripotiwa katika miji mingine mikubwa ya Algeria kama vile Constantine, Annaba na Bilda. Bouteflika amekuwa madarakani kwa muda wa miaka 20 sasa na hajawahi kuzungumza hadharani tokea apate kiharusi mwaka 2013.
Vijana sasa ndio walio katika mstari wa mbele wa maandamano nchini Algeria na wanataka kizazi kipya cha viongozi wapewe fursa ya kutawala.  Bouteflika anayekabiliwa na upinzani wa umma amesema atagombea tena urais kwa mara ya tano katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Aprili lakini amebaini kuwa hatamaliza muhula wake wote. Hata hivyo waandamanaji wamepinga vikali pendekezo hilo na wanataka aondoke
Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria
Wakati huo huo Jeshi la Algeria limesema litadhamini usalama na halitaruhusu nchi hiyo irejee katika zama za umwagikaji damu. Akizungumza Jumanne, Mkuu wa Majeshi ya Algeria, Luteni Jenerali Ahmed Gaid Salah, bila kutaja majina, amesema kuna wale ambao wanataka nchi hiyo irejee katika "miaka ya machungu", akiashiria vita vya ndani nchini humo katika muongo wa 90.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages