LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 24, 2019

WASENEGARI WAPIGA KURA

Muda mfupi baada ya kupiga kura katika eneo la Fatick, katikati mwa nchi, Sall amesema, "ushindi katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais ni wetu, na hilo halipingiki."
Watetezi wa haki na wakosoaji wa serikali ya Senegal wameitaja hatua ya kuzuiwa kushiriki uchaguzi huo washindani wakuu wa Rais Sall kuwa ni ukandamizaji wa kutisha dhidi ya wapinzani.
Shakhsia hao wa upinzani waliozuiwa kuchuana na Sall ni Khalifa Sall ambaye amewahi kuwa Meya wa mji mkuu Dakar na Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa nchi hiyo.

Uchaguzi wa Rais wa Senegal 2019

Sall mwenye umri wa miaka 57 alianza siasa akiwa mwanachama wa chama kilichokuwa kikiongozwa na Wade cha Senegalese Democratic Party (PDS) na kisha baina ya mwaka 2004 na 2007  akawa Waziri Mkuu wake, kabla ya kuwa rais wa nchi hiyo mwaka 2012.
Katika uchaguzi wa leo, Sall anachuana na wagombea ambao wachambuzi wa kisiasa wanawataja kuwa 'dhaifu' ambao ni Idrissa Seck, Waziri Mkuu wa zamani, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Madicke Niang, Issa Sall wa chama cha PUR na Ousman Sonko ambaye amewahi kuwa Mkuu wa Mamlaka ya Ushuru na pia mbunge.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages