LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 2, 2019

OLE SENDEKA AZINDUA OPARESHEN MAALUM YA KUWASAKA WAUWAJI WA WATOTO NJOMBE

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amezindua oparesheni maalum ya kuwasaka watuhumiwa wa mauaji ya watoto katika Mkoa wa Njombe kufuatia kuongezeka kwa mauaji ya watoto kwenye mkoa huo.



Kauli hiyo inakuja kufuatia kutokea kwa mauaji ya watoto 9 ambapo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole-Sendeka amebainisha kuwa ikitokea tukio hilo familia nzima zitahusishwa  pamoja na viongozi wa eneo husika.

Ole Sendeka amesema "hata kama ulipigiwa simu tutaifuatilia simu yako, utatuunganisha na utatueleza mahusiano yako na huyo mtu na haya anayoyafanya ukijifanya kukataa tutakuunganisha kwenye mauaji ya watoto."

"Tungependa kuanza na  hawa ambao ni matajiri wanaoaminika walipata utajiri kwa njia ambazo si halali watatusaidia na tutawashika ili kuisaidia Jeshi la Polisi." ameongeza Ole Sendeka

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages