Hospitali ya Taifa Muhimbili, tawi la Mloganzila (MAMC), imeanza kutoa huduma ya kisasa ya uchunguzi wa saratani ya matiti.
Kwa njia hiyo ya kisasa, wataalamu sasa wanao uwezo wa kuchukua sampuli ya kinyama (biopsy) mwilini pasipo kufanya upasuaji wa aina yoyote ile.
Mtaalamu wa Tiba Mionzi (Radiologist), Dk. Lulu Sakafu amesema hayo leo Februari 2, alipozungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo.
Amesema hiyo ni mara ya kwanza kwa huduma hiyo kuanza kutolewa hospitalini hapo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇