Katika kuendeleza uingiliaji wake katika siasa za nje za Uturuki, Marekani imeionya Ankara dhidi ya kushirikiana na serikali halali ya Venezuela.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo serikali ya Marekani imeionya Uturuki kutokana na kuiunga mkono serikali ya Rais Nicolás Maduro wa Venezuela na kwamba hadi sasa haijapata jibu chanya kutoka kwa Ankara kuhusu kushirikiana na Marekani kuiondoa madarakani serikali ya Caracas. Hata hivyo bado Uturuki haijatoa msimamo wake kuhusiana na vitisho hivyo vya Washington dhidi yake. Katika miaka ya hivi karibuni Uturuki imeimarisha uhusiano wake wa kibiashara na serikali ya Venezuela.
Uturuki ni miongoni mwa nchi ambazo zimetangaza wazi msimamo wao katika kupinga uingiliaji wa Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya katika masuala ya ndani ya Venezuela. Ni siku kadhaa sasa ambapo Marekani na washirika wake sambamba na kumuunga mkono kiongoni wa upinzani wa serikali ya Venezuela, zimekuwa pia zikifanya njama za kila namna kutekeleza mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇