LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 2, 2019

RAIS DK. MAGUFULI AMJULIA HALI CHARLES KITWANGA ALIYELAZWA MUHIMBILI

MUHIMBILI, DSM
Rais wa Dk. John Magufuli leo amemjulia hali Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe. Charles Kitwanga ambaye amelazwa wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam akipatiwa matibabu.

Kitwanga ambaye amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, amelazwa hospitalini hapo tangu juzi, tarehe 31 Januari, 2019 ambako alihamishiwa kutoka Dodoma.

Kwa mujibu wa Ikulu, Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya dharura na ajali Dk. Juma Mfinanga amemueleza Rais Magufuli kuwa hali ya Kitwanga inaendelea vizuri ikilinganishwa na wakati alipofika hospitalini hapo juzi.

Akiwa wodini hapo Rais Magufuli ameshiriki sala ya kumuombea Kitwanga ilia pone haraka na amewashukuru Madaktari na Wauguzi kwa juhudi kubwa wanazozifanya kuwahudumia wagonjwa.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages