Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu amesema serikali ipo tayari kurejesha kwa wananchi mashamba yenye Malalamiko katika hifadhi ya Msitu ya Igwata Wilayani Maswa Mkoani Simiyu.
Kanyasu ameyasema hayo leo Februari 8 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Maswa Magharibi Mashimba Mashauri Ndaki aliyetaka kujua kwanini serikali isirejeshe mashamba yaliyomegwa kutoka wananchi ili waendelee na shughuli za kilimo.
Katika majibu yake Naibu waziri Costantine amesema zoezi linaloendelea katika wizara ya Maliasili na utalii ni kurejesha kwa wananchi maeneo yenye malalamiko .
Msitu wa hifadhi wa Igwata unahifadhiwa kisheria kwa tangazo la kiserikali No.324 la mwaka 1953 ukiwa na ukubwa wa eneo la hekta laki 1 elfu 32,mia 4 na 51 ambapo hekta 85.19 zipo wilaya ya Kwimba na hekta 47.678 zipo wilaya ya Maswa huku wakala wa mistu Tanzania TFS ilianza kusimamia msitu wa Igwata rasmi tangu mwaka 2010 hadi sasa.
Wakati huohuo waziri wa Maliasili na Utalii Dokta Hamis Kigwangalla amepiga marufu usafirishaji wa wanyama hai nje ya nchi kuanzia sasa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇