Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeombwa na Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera kuongeza umakini katika usimamizi wa ligi ili apatikane bingwa halali.
Kocha huyo amesema ligi ya Tanzania ni bora lakini imepoteza ushindani kutokana na mambo ya ovyo yanayoendelea kufanyika ndani ya ligi na kupelekea kupunguza ushindani.
“Hiyo haina ubishi kama ligi itachezwa kwa haki na usawa basi timu yoyote itakayokuwa bingwa basi itafanya vizuri ndani na nje ya nchi lakini kwa mfumo wa sasa wa ligi ni ngumu kupatikana mwakilishi mzuri “ alisema Zahera.
Zahera amesema utakuta waamuzi wanachezesha huku wakilazimisha timu A ifunge timu B wakati hawana uwezo.
“Kuna nchi ambazo zinawashiriki zaidi ya watatu katika mashindano ya Kimataifa kama DRC Congo, Misri, Zambia pamoja na Morocco ambapo mbili zinacheza ligi ya mabingwa Afrika na moja au mbili zinacheza Kombe la Shirikisho hayo ndiyo maendeleo ya soka,”alisema Zahera.
Alisema inatakiwa kufika kipindi Biashara United kuifunga Yanga SC au Simba SC isiwe stori lichukuliwe kama tukio la kawaida kwenye soka
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇