LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 15, 2019

CHINA YAIKABIDHI IKULU MPYA BUFUNDI

Balozi wa China nchini Burundi, Li Changlin na waziri wa mambo ya nje wa Burundi, Ezechiel Nibigira wamesaini hati ya makabidhiano ya jengo la Ikulu ya Burundi lililojengwa kwa msaada wa China.


Kwenye hafla ya kusaini hati ya makabidhiano kwenye Ikulu mpya kwenye eneo la Mutimbuzi, kaskazini mwa Bujumbura, balozi wa China, Li Changlin amesema makabidhiano hayo ni alama ya urafiki na ushirikiano kati ya China na Burundi, na kwamba ushirikiano kati ya nchi hizo mbili utaweka mkazo katika kuboresha maisha ya wananchi wa Burundi na mazingira ya kazi ya watumishi wa umma wa Burundi.

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi, Nibigira ameishukuru China kwa kujenga Ikulu hiyo, ambayo Burundi haijawahi kuwa nayo tangu ijipatie uhuru mwaka 1962, na kusema kwamba hii ni mara ya kwanza katika historia kwa Burundi kupata miundombinu mizuri, na imethibitisha uhusiano imara wa kisiasa na kidiplomasia uliopo kati ya Burundi na China.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages