Mwanamke mmoja mkazi wa Kijichi Mkoa wa Mjini Magharibi, amedai kupigwa na kujeruhiwa usoni na mumewe ambapo ameshonwa nyuzi 6, kwa madai ya kukataa kuingiliwa kinyume na maumbile na mumewe huyo.
Amesema kwa muda sasa mumewe amekuwa akimtaka kinyume na maumbile, akimshutumu kuwa hajui mapenzi.
Mwanamke huyo amesema kuwa Mume wake alianza kumuomba penzi kinyume na maumbile miezi mitatu baada ya kumuoa.
Baada ya kuweka msimamo huo, Mume wake alianza kumtukana na kumwambia hajui mapenzi ambapo majirani walimueleza kuwa hiyo ndiyo tabia ya mwanaume huyo na ndiyo sababu ya kuachana na wake zake wawili.
Hata hivyo mwanaume huyo amekana taarifa hizo na kudai kuwa chanzo cha mgogoro wake na mkewe ni wakwe zake wanaomdai mahari kwa kumsimanga.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇