Baraza la wawakilishi nchini Marekani limeidhinisha Februari 13 mwaka huu azimio litakalofikisha mwisho uungaji mkono wa Marekani kwa muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita nchini Yemen.
Hatua hiyo imechukuliwa wakati wabunge wengi wakitaka kumlazimisha rais Donald Trump kuimarisha sera zake kuelekea nchi hiyo ya Kifalme.
Ilikuwa mara ya kwanza baraza hilo la wawakilishi kuunga mkono azimio la madaraka ya vita, lakini kura hiyo iliyoungwa mkono na wabunge 248 kwa 177 waliopinga, kwa karibu kwa misingi ya kichama, haitatosha, hata hivyo, kuweza kuikiuka ahadi ya Trump kutoa kile ambacho kinaweza kuwa kura yake ya kwanza ya turufu.
Wabunge 18 tu wa chama cha Trump cha Republican katika baraza hilo la wawakilishi waliojiunga na Wademokrati 230 kuunga mkono azimio linalotaka kuzuwia jeshi la Marekani kujiingiza katika uhasama ndani ama inayoiathiri Yemen, ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa kujaza mafuta katika ndege zinazofanya mashambulizi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Yemen, bila ya idhini kutoka katika bunge la Marekani Congress.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇