LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 1, 2019

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.SHEIN ASHIRIKI TAMASHA LA MAZOEZI KISIWANI PEMBA LEO ASUBUHI.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanya Mazoezi ya Viungo Zanzibar Ndg,Said. Suleiman akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazoezi Kitaifa yaliofanyika katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.(PICHA NA IKULU)

Kamishna wa Michezo Zanzibar. Bi.Sharifa Khamis akizungumza wakati  Tamasha la Mazoezi katika Viwanja vya Gombani leo asubuhi.1-1-2019.

Waziri wa Vijana Michezo Utamaduni na Sanaa Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume akizungumza wakati wa Tamasha hilo kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kuzungumza na Wananamichezo katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wanamichezo wa Vikundi vya Mazoezi wakati wa Tamasha la Kitaifa la Michezo ya lililofanyika katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba leo asubuhi 1-1-2019.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Cheti cha Shukrani kilichotolewa na Chama Cha Wanamichezo ya Viungo Zanzibar Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Ndg Abdalla Juma.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Cheti cha Shukrani Mjumbe wa Chama cha Mazoezi ya Viungo Zanzibar ,kupitia Jumuiya wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar Ndg. Haidar Madoweya, wakati wa hafla hiyo ya mazoezi iliofanyika Uwanja wa Gombani Pemba.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Cheti cha Shukrani kwa Kushiriki katika Tamasha la Mazoezi Kiongozi wa ZONE B Unguja Dau Hamad. Kulia Waziri wa Vijana Michezo Utamaduni na Sanaa Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages