Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa iliyopo Kata ya Nachingwea katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa kuzindua madarasa mawili yaliyojengwa na Benki hiyo kwa gharama ya shilingi milioni 80, Desemba 31, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kisalimiana na baadhi ya viongozi na watendaji wa Benki ya CRDB wakati alipowasili kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa kuzindua madarasa mawili yaliyojengwa na benki hiyo kwenye Kata ya Nachingwea katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa kwa gharama ya Shilingi milioni 80, Desemba 31, 2018. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay na watatu kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua madarasa mawili yaliyojengwa na Benki ya CRDB kwa gaharama ya shilingi milioni 80 katika Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa kwenye Kata ya Nachingwea iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Desemba 31, 2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Ngandirwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua madarasa mawili yaliyojengwa na Benki ya CRDB kwa gaharama ya shilingi milioni 80 katika Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa iliyopo Kata ya Nachingwea katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kulia ni Mkewe Mary, wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally Hussein Laay na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (watatu kushoto) wakiwa katika moja ya madarasa mawili yaliyojengwa na Benki ya CRDB kwa gaharama ya shilingi milioni 80 katika Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa iliyopo Kata ya Nachingwea katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa na kuzinduliwa na Waziri Mkuu, Desemba 31, 2018. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela, Mwanfunzi wa Kidato cha Pili katika Shule hiyo, Mwanahawa Choni, Khadija Abdallah wa Kidato cha Pili katika Shule hiyo na Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally Hussein Laay.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay (kushoto kwake) kukagua madarasa mawili aliyoyazindua katika Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa iliyopo kwenye Kata ya Nachingwea katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Desemba 31, 2018. Madarasa hayo yamejengwa na CRDB kwa gharama ya shilingi milioni 80.
Waalikwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuzindua madarasa mawili yaliyojengwa na Benki ya CRDB kwa gharama ya shilingi milioni 80 katika Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa kwenye Kata ya Nachingwea katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Desemba 31, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuzindua madarasa mawili yaliyojengwa na Benki ya CRDB kwa gaharama ya shilingi milioni 80 katika Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa katika Kata ya Nachingwea kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kushoto ni Mkewe Mary, Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally Hussein Laay na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
NA OWM, NACHINGWEA
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amepokea msaada wa vyumba viwili vya madarasa vikiwa na madawati vyenye thamani ya sh. milioni 80 kutoka kwa bank ya CRDB.
Alipokea madarasa hayo jana (Jumatatu, Desemba 31, 2018) katika shule ya Sekondari Kassim Majaliwa iliyopo Kata ya Nachingwea katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi
Waziri Mkuu aliushukuru uongozi wa benki ya CRDB kwa msaada hu ambao umesaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa madarasa unaoikabili wilaya hiyo.
Kadhalika, Waziri Mkuu alizitaka taasisi nyingine ziige mfano wa bank ya CRDB kwani imekuwa bega kwa bega na Serikali katika kuchangia shughuli za kimaendeleo nchini.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alitoa wito kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Kassim Majaliwa kutumia vizuri madarasa hayo na kutunza mali zilizopo shuleni hapo.
Alisema ujenzi wa shule hiyo ni mradi uliobuniwa na wakazi wa kata ya Nachingwea ili kuwawezesha watoto wao kupata elimu katika eneo lililo karibu na makazi yao.
Waziri Mkuu alisema awali wanafunzi wa kata hiyo walikuwa wanatembea umbali mrefu hadi shule ya sekondari ya Ruangwa jambo ambalo lilikuwa ni changamoto kwao.
“Nawaomba wananchi wenzangu tuendelee kushirikiana katika kuibua na kubuni miradi mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maendeleo kwenye kata yetu ya Nachingwea.”
Pia Waziri Mkuu alikabidhi kompyuta 20 kwa shule za sekondari tano ambazo ni Kassim Majaliwa, Likunja, Mnacho, Hawa Mchopa na Ruangwa.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema benki yao inathamini elimu na imekuwa ikirudisha kwa jamii faida wanayoipata kwa kuchangia shughuli za maendeleo.
Alisema mbali na msaada huo wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na madawati yake, pia aliahidi kutoa sh. milioni 20 ili zitumike kununulia madawati yatakayosaidia kupunguza changamoto ya madawati wilayani Ruangwa.
Kwa upande wao, wakazi wa kata ya Nachingwea wilayani Ruangwa waliishukuru Serikali kwa kuwaunga mkono katika mradi wa ujenzi wa shule hiyo ya sekondari ambayo imewawezesha watoto wao kusoma karibu na maeneo yao ya makazi yao.
Mmoja wa wakazi hao Omari Losi alisema ujenzi wa shule hiyo utawarahisishia wanafunzi kwenda shule na kuwaondolea shida ya kutembea umbali mrefu kwenda shule ya sekondari ya Ruangwa walikokuwa wakisoma awali.
Naye, mkazi mwingine wa kata hiyo ya Nachingwea, Mariam Kingamkono alisema uwepo wa shule ya sekondari katika kata yao kumeongeza hamasa ya wanafunzi kupenda kusoma kwa sababu wameondolea shida ya kutembea umbali mrefu.
Alisema shule hiyo inawalimu wazuri na wa kutosha na ina mazingira mazuri ya kujifunzia, hivyo aliwaomba wazazi wenzake waendelee kushirikiana na Serikali katika kuboresha maendeleo kwenye kata yao hususan ujenzi wa shule.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇