LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 8, 2019

PAPA FRANCIS ATAHADHARISHA KUHUSU HATARI YA KUTOKEA VITA VYA TATU VYA DUNIA

  • Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ametahadharisha kuhusu hatari ya kutokea vita vingine vya dunia.
Akizungumza jana mbele ya kikao cha mabalozi wa nchi za kigeni huko Vatican katika hotuba yake ya kila mwaka, Papa Francis ameashiria machafuko yanayotawala maeneo mbalimbali ya dunia na kusema kuwa, kuendelea kwa mwenendo wa sasa wa kuhatarishwa sera ya ulimwengu wa kambi kadhaa, kunaiweka dunia katika ncha ya vita vya tatu vya dunia. 
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amesema kuwa, kuna udharura wa kuimarishwa irada na azma ya kufanyika mazungumzo ya amani na yenye tija baina ya nchi mbalimbali na kuongeza kuwa: Kutokana na hali ya sasa fikra za utaifa zinahatarisha kazi za jumuiya za kimataifa.
Papa Francis amezungumzia pia kadhia ya wahajiri na kukumbusha matokeo ya kukatisha tamaa ya makubaliano ya kimataifa ya wahajiri mwezi uliopita nchini Morocco ambayo nchi nyingi ikiwemo Italia zimekataa kuyasaini.
Papa Francis 
Kiongozi wa Kanisa Katoliki ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za dharura za kukubaliwa wahajiri katika jamii za nchi zilizowapokea na kusisitiza kuwa, kuna umuhimu wa kuchukuliwa hatua ili watu hawa wasilazimike kuacha familia na nchi zao au warejeshwe katika nchi walikotoka kwa heshima na kuzingatiwa haki zao za kibinadamu.
Vilevile amezungumzia unyanyasaji wa kingoni dhidi ya watoto unaofanywa na makasisi na viongozi wa kidini akiutaja kuwa ni miongoni mwa madhara makubwa ya kipindi cha sasa. Papa Francis amesema kuwa mkutano muhimu wa maaskofu utakaofanyika mwezi ujao wa Februari huko Vatican utamulika kikamilifu uhakika wa mambo kuhusu kadhia hiyo na njia za kuhafifisha majeraha yaliyosababishwa na uhalifu huo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages