LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 8, 2019

WALIMU ZIMBABWE KUANZA MGOMO JUMANNE HII KUHUSU MISHAHARA YAO

Walimu nchini Zimbabwe wamesema kuwa leo Jumanne wanaanza mgomo kushinikiza kulipwa mishahara yao kwa sarafu ya dola ya Kimarekani. Hayo yameelezwa na muungano wa walimu wa nchi hiyo.
Walimu nchini Zimbabwe wametangaza kuanza mgomo huo huku Rais wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa akiendelea kukabiliwa na mashinikizo ili kuipatia ufumbuzi hali ya kiuchumi inayolegalega sasa nchini humo. Uhaba wa fedha umeyumbisha mfumo wa fedha wa Zimbabwe na kuzidisha uwezekano wa kuibuka ghasia. Kulegalega huko kwa hali ya uchumi Zimbabwe kunarudisha nyuma juhudi za Rais Mnangagwa za kuwavutia wawekezaji wa nje ambao waliwekwa kando wakati wa utawala wa Rais Robert Mugabe.
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe 
Muungano wa Walimu wa Zimbabwe (ZIMTA) umesema kuwa wanachama wake watafanya mgomo huo kutokana na kupanda kwa gharama za maisha ikiwemo ongezeko la bei ya bidhaa; jambo linalowapelekea kushindwa kukidhi mahitaji yao ya msingi.
Itakumbukwa kuwa madaktari Zimbabwe sasa wanaendelea kugoma kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu kuhusiana na suala hilo hilo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages