Na Scolastica Msewa, Kibaha.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa (pichani), amesema hakuna korosho za wakulima nchini zitakazobaki bila ya kununuliwa.
Ameyasema hayo jana alipozungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha korosho cha Terra kilichopo Kibaha wakati alipofanya ziara ya siku moja.mkoani pwani ambapo pia alitembelea kianda cha Kutengeneza marumaru cha Keda Na kiwanda cha Juisi cha Sayona.
amewaambia wananchi na wakulima wa korosho nchini baada na kuwahakikishia kuwa korosho zao zote zitanunuliwa.
Amesema Serikali kupitia Bodi ya Mazao Mchanganyiko itanunua korosho zote na hakuna korosho za wakulima nchini ambazo zitabaki bila ya kununuliwa.
Ameyasema hayo jana alipozungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha korosho cha Terra akiwa njiani kwenda Dodoma.
Waziri Mkuu amesema bodi hiyo inaendelea kufanya thamini na kujiridhisha kama kweli korosho hizo zimezalishwa nchini na kuangalia viwango vya ubora.
Amesema baada ya kujiridhisha kuhusu viwango vya ubora na mkulima aliyepeleka ndiye mwenyewe ndipo taratibu za malipo hufanyika.
Waziri Mkuu amesema Serikali iliamua kununua korosho baada ya wafanyabiashara kutaka kuzinunua kwa bei ya chini ambayo haikuwa na tija.
“Lengo la Serikali ni kuhakikisha mkulima ananufaika na ndipo Rais Dkt. John Magufuli alisitisha ununuzi baada ya kuona wakulima wanataka kudhulumiwa.”
Waziri Mkuu amesema kuwa hadi sasa tayari tani 181,000 zimeshakusanywa, hivyo amewataka wakulima wa zao hilo nchini waendelee kuiamini Serikali yao.
Kadhalika, Waziri Mkuu ameupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuunga mkono jitihada za Serikali kukuza uchumi kwa kupitia sekta viwanda.
Meneja Utawala wa kiwanda cha Terra, Peter Christopher alisema uwezo wao ni kubangua tani 6,000 kwa mwaka, ambapo tayari wamebangua tano 3,000.
Pia aliiomba Serikali iwasaidie katika suala la ubora wa korosho kwa kuwa kiwango cha ubora kinachoandikwa kinakuwa tofauti na uhalisia wa korosho yenyewe.
Akiwa ktk kiwanda cha kutengeneza marumaru cha KEDA kilichopo Chalinze Waziri Mkuu alipongeza uzalishaji mkubwa wa marumaru Na kusema ni za viwango vya ubora Na Thamani kubwa inayoongoza Africa mashariki.
lisema kuwa wakati Serikali ikiendelea kukaribisha wawekezaji hasa katika nyanja za Viwanda kumekuwa na fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo zimeendelea kujitokeza na kinachotakiwa ni wananchi kuzitumi ili kujikwamua kiuchumi.
"Hivi Viwanda vitahitaji malighafi na malighafi zinaletwa na wageni Kutoka Mikoani hivyo mkijenga mahotel na nyumba za kulala wageni mtakuwa mmejiwekea fursa ya kiuchumi watalala,watakula watakunywa soda na maji mtakuwa mmepata pesa"alisema
Akiwa kwenye Kiwanda cha kubangua korosho cha Terra Cashew Tanita Kibaha alisema Serikali kupitia Bodi ya Mazao Mchanganyiko itanunua korosho zote za wakulima nchini na kuwalipa Pesa zao kulingana na bei iliyopo.
“Lengo la Serikali ni kuhakikisha mkulima ananufaika na ndipo Rais . John Magufuli alisitisha ununuzi wa korosho uliokuwa unawakandamza wakulima na kuweka utaratibu uliopo Sasa"alisema
Awali Meneja Utawala wa kiwanda cha kubangua korosho cha Terra Cashew kilichoko Tanita Kibaha Peter Christopher alisema uwezo wao ni kubangua tani 6,000 kwa mwaka, ambapo tayari wamebangua tano 3,000.hivyo wana uhakika wa kufanya kazi hiyo kwa uhakika.
Pia aliiomba Serikali iwasaidie katika suala la ubora wa korosho kwa kuwa kiwango cha ubora kinachoandikwa kwenye magunia kinakuwa tofauti na uhalisia wa korosho zenyewe.
Mmoja wa wamiliki wa Kiwanda cha kutengeneza vigae cha Keda kilichoko Chalinze Tony Wu akitoa taarifa yake kwa Waziri Mkuu alisema kuwa mpana Sasa wametoa ajira rasmi kwa watanzania zaidi ya 1000 huku zaidi ya 3000 wakipata ajira zisizorasmi na kwamba wataendelea kutoa fursa hiyo kadri wanavyoendelea na upanuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alisema kuwa mpaka Sasa Mkoa wa Pwani una jumla ya Viwanda vikubwa 109 vya aina mbalimbali huku wakiwa wanaendelea kukaribisha wawekezaji kwa kutenga maeneo makubwa ya ardhi.
Your Ad Spot
Dec 8, 2018
Home
Unlabelled
SERIKALI YASEMA HAKUNA KOROSHO ZA WAKULIMA ZITAKAZOKOSA KUNUNULIWA
SERIKALI YASEMA HAKUNA KOROSHO ZA WAKULIMA ZITAKAZOKOSA KUNUNULIWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇