Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi, amewataka masheikh na viongozi wa dini ya Kiislamu nchini humo kukemea vitendo vya ushoga.
Mufti wa Tanzania ameyasema hayo katika hafla ya Baraza la Maulidi ya kukumbuka tukio la kuzaliwa Mtume Muhammad (saw), ambayo yamefanyika kitaifa, wilayani Korogwe mkoani Tanga na kuongeza kwamba, ushoga haukubaliki nchini Tanzania na unatakiwa kupingwa kwa nguvu zote. “Jambo la ushoga halikubaliki, haiwezekani nchi tukufu kama Tanzania kuwa na vitendo hivi. Masheikh lisemeni jambo hili ili tunusuru umma na taifa kwa ujumla.” Amesema Mufti wa Tanzania. Baraza la Maulidi ya kukumbuka tukio la kuzaliwa Mtume Muhammad (saw), limeongozwa na Waziri wa Nchi Tamisemi, Seleman Jafo ambaye amemuwakilisha Rais John Pombe Magufuli na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na serikali.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇